Trump asema jeshi la Marekani lashambulia IS kaskazini magharibi mwa Nigeria

(CRI Online) Desemba 26, 2025

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kwamba jeshi la Marekani lilifanya shambulio kubwa dhidi ya wapiganaji wa IS kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Truth Trump alisema chini ya maelekezo yake kama Amiri Jeshi Mkuu, Marekani ilishambulia wahalifu hao wa kigaidi wa ISIS, ambao wamekuwa wakiwalenga na kuwaua kikatili, hasa Wakristo wasio na hatia, katika viwango ambavyo havijaonekana kwa miaka mingi, na hata karne.

Aidha Trump ameongeza kuwa Idara ya Vita ilitekeleza mashambulizi mengi kamili, akiapa kwamba Marekani haitaruhusu ugaidi wa msimamo mkali wa Kiislamu kufanikiwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha