Lugha Nyingine
China yahizima Marekani kuacha kutekeleza vifungu hasi vinavyohusiana na China katika Mswada wa Sheria ya Uidhinishaji wa Ulinzi wa Taifa
BEIJING, Desemba 25 — Msemaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Umma la China (NPC) Xu Dong Alhamisi amesema kuwa, hivi karibuni “Mswada wa Sheria ya Uidhinishaji wa Ulinzi wa Taifa ya Mwaka wa Fedha 2026” uliopitishwa kwenye Bunge la Marekani umetiwa saini na kuwa sheria, ambayo inahusisha mambo hasi yanayohusu China. Sheria hiyo inaendelea kufuata mtazamo wake wa siku zote wa kuzuia China, ikitia chumvi “tishio la China”, kuingilia kijeuri kati ya mambo ya ndani ya China, na kudhuru maslahi ya kiini ya China. Tunalalamika vikali na kuipinga kithabiti.
Tunatumai upande wa Marekani kuwa na mtazamo wa kufuata hali halisi juu ya maendeleo ya China na uhusiano kati ya China na Marekani, na kuelekea China kwa njia sahihi, ili kutekeleza vitendoni kwa pamoja makubaliano muhimu yaliyofikiwa na marais wa China na Marekani katika mkutano wa Busan.
Tunahimiza upande wa Marekani kuacha mtazamo wa mchezo wa kutiana hasara na maoni ya itikadi ya upande wake mmoja, na kutotekeleza vifungu hasi vinavyohusu China vilivyomo kwenye sheria hiyo. Kama Marekani itaendelea kufuata njia yake pekee, China itachukua hatua zenye nguvu kwa mujibu wa sheria ili kulinda kwa uthabiti mamlaka ya nchi na maslahi ya maendeleo na usalama.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



