Mradi wa taa za barabarani ulioungwa mkono na China wang’arisha mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi

(CRI Online) Desemba 29, 2025

(Picha inatoka tovuti ya Ubalozi wa China nchini Burundi.)

(Picha inatoka tovuti ya Ubalozi wa China nchini Burundi.)

Mradi wa taa za barabarani zinazotumia nishati ya jua ulioungwa mkono na China umekamilika katika mji mkuu wa kiuchumi wa Burundi, Bujumbura, na kuendana na dira ya nchi hiyo ya kuhimiza nishati safi, ufanisi wa nishati, na maendeleo endelevu, amesema Martin Ndayizeye, Katibu Mkuu katika Wizara ya Nishati na Madini, Viwanda, Biashara, na Utalii ya Burundi.

Mradi huo ulioungwa mkono na Mkoa wa Sichuan wa China, umetekelezwa kwenye Barabara ya Mao Zedong katika Wilaya ya Mukaza mjini Bujumbura, ambayo kwa sasa ina taa 101 za barabarani zinazotumia nishati ya jua ambazo zinajiwasha na kujizima kiotomatiki kulingana na kiwango cha mwanga wa asili.

“Muundombinu huu wa kisasa na endelevu ni hatua muhimu ya kuleta usasa kwenye mji mkuu wetu wa kibiashara (Bujumbura)” amesema Ndayizeye.

Huku akiipongeza China kuwa ni “mshirika wa kimkakati na mwenye kuaminika” wa Burundi, Ndayizeye amebainisha kuwa “uungaji mkono huu wa kikarimu unaonesha tena uhusiano bora wa ushirikiano na urafiki kati ya Burundi na China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha