Lugha Nyingine
Mvua kubwa yavuruga safari za treni ya SGR nchini Tanzania
(CRI Online) Desemba 30, 2025
Wasafiri wanaotumia reli ya SGR nchini Tanzania walikwama kwa saa kadhaa siku ya Jumapili kwenye stesheni ya Magufuli jijini Dar es Salaam baada ya huduma kusitishwa kutokana na changamoto za kiufundi zilizosababishwa na mvua kubwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Machibya Masanja amesema, mvua hizo zimesababisha hitilafu za kiufundi ndani ya mfumo wa reli, na kuwalazimu mafundi kusimamisha kwa muda uendeshaji wa huduma ili kuruhusu ukaguzi wa usalama na matengenezo.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Jumapili ilitoa tahadhari ya mvua kubwa katika maeneo mengi ya nchi hiyo, na kuonya mwendelezo wa hali mbaya ya hewa na athari zinazotokana na hali hiyo katika miundombinu na usafiri.
(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



