Malawi yaomba uungaji mkono wa dola za kimarekani milioni 3 ili kupambana dhidi ya mlipuko wa kipindupindu

(CRI Online) Desemba 30, 2025

Serikali ya Malawi Jumapili ilitoa ombi la uungaji mkono wa kifedha wa dola zaidi ya milioni 3 za kimarekani ili kutekeleza mpango wa nchi hiyo wa kudhibiti kipindupindu.

Akizungumza na wanahabari mjini Lilongwe, Waziri wa Afya wa nchi hiyo Madalitso Baloyi amesema kesi za watu 11 waliothibitishwa kuugua ugonjwa wa kipindupindu zimerekodiwa katika wilaya tano za nchi hiyo, ikiwemo Lilongwe.

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imesema, serikali ya Malawi imeimarisha uratibu wa kuvuka mpaka na uchunguzi wa pamoja wa kuvuka mpaka wa kesi za watu wanaoshukiwa kuugua katika wilaya mbili za mpakani za Mwanza na Moatize nchini Msumbiji.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha