Lugha Nyingine
Russia yasema Ukraine imefanya shambulizi la droni kwenye makazi ya rais huko Novgorod
Waziri wa mambo ya nje ya Russia Sergei Lavrov amesema kuwa Ukraine imefanya shambulizi la droni kwenye makazi ya rais katika eneo la Novgorod, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
"Katika usiku wa Desemba 28 hadi 29, serikali ya Ukraine ilianzisha shambulizi kwa kutumia droni 91 za mashambulizi ya masafa marefu kwenye eneo la makazi ya Rais wa Shirikisho la Russia" Lavrov alisema jana Jumatatu.
Amesema droni zote zilizorushwa ziliangushwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Jeshi la Russia na hakuna ripoti yoyote ya majeruhi wala uharibifu kutokana na shambulizi hilo.
Waziri Lavrov amesisitiza kuwa shambulizi hilo limetokea huku kukiwa na mazungumzo mapana kati ya Russia na Marekani yanayolenga kutatua mgogoro huo wa Ukraine.
Ameonya kuwa kitendo hicho hakitapita bila ya kujibiwa, huku akithibitisha kuwa Jeshi la Russia limeshabainisha maeneo lengwa kwa ajili ya mashambulizi ya kulipiza kisasi na kupanga ratiba kwa ajili ya utekelezaji wake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



