Lugha Nyingine
PLA yafanya mazoezi kuizunguka Taiwan ili kuzuia nguvu ya mafarakano ya kutaka "Taiwan Ijitenge" na uingiliaji wa nje
NANJING/BEIJING - Eneo la Kivita la Mashariki la Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) jana Jumatatu lilifanya mazoezi makubwa pamoja ya kijeshi kuzunguka Kisiwa cha Taiwan, yanayojulikana kwa jina la msimbo "Operesheni ya Haki 2025."
Shi Yi, Msemaji wa Eneo hilo amesema kwamba mazoezi hayo yanahusisha vitengo vya Jeshi, Kikosi cha Majini, Kikosi cha Anga, na Kikosi cha Roketi vinavyotekeleza operesheni kwenye Mlango-Bahari wa Taiwan na maji ya kaskazini, kusini-magharibi, kusini-mashariki, na mashariki mwa kisiwa hicho.
Ni onyo kali dhidi ya shughuli za kutaka "Taiwan Ijitenge" na uingiliaji wa nje, Shi amesema, akiongeza kuwa mazoezi hayo ni hatua halali na muhimu ya kulinda mamlaka na umoja wa kitaifa wa China.
Kwa mujibu wa Shi, mazoezi hayo yanalenga doria ya utayari wa mapigano ya baharini na angani, kupata ubora wa kijeshi katika pande zote, kufunga bandari na maeneo muhimu, vilevile kuimarisha uwezo wa kuzuia pande zote nje ya mnyororo wa visiwa.
Jana Jumatatu, huku meli na ndege za kivita zikikaribia Kisiwa cha Taiwan kutoka pande tofauti, wanajeshi wa huduma mbalimbali walitekeleza mashambulizi ya pamoja ili kujaribu uwezo wao wa operesheni za pamoja.
Kwenye maji na anga katika maeneo ya katikati ya Mlango-Bahari wa Taiwan, eneo hilo la kivita lilitumia ndege za kivita, ndege za kubeba mabomu, na ndege zisizo na rubani kwa kushirikiana na urushaji wa makombora ya masafa marefu ili kufanya mazoezi ya kushambulia maeneo lengwa ya ardhini yanayoweza kuhamishika.
Kwenye upande wa mashariki wa Kisiwa cha Taiwan, manowari za kuharibu, manowari za frigeti, ndege za kivita, na za kubeba mabomu zilitekeleza mazoezi ya kushambulia maeneo lengwa ya baharini, kutawala anga za kikanda, vilevile uwindaji wa nyambizi na operesheni za kupambana na nyambizi. Eneo hilo pia lilituma vikosi maalumu vya ndege za kurusha makombora kufanya doria za utayari wa mapigano kwenye bahari za mbali katika eneo hilo, vikijikita katika mashambulizi ya anga kutoka umbali na mashambulizi ya pamoja ya kulenga kwa usahihi.
Wakati huo huo, kwenye maji na anga za upande wa kaskazini na kusini-magharibi mwa kisiwa hicho, manowari za kuharibu, manowari za frigate, ndege za kivita, za kubeba mabomu, na ndege zisizo na rubani vilitekeleza mara nyingine tena mazoezi ya kurusha kwa ushirikiano na roketi za masafa marefu.
Shi amesema, mazoezi hayo yalihusu kutafuta na kubomoa maeneo lengwa kote majini na angani, kuigilizia mashambulizi kwenye maeneo lengwa ya ardhini, na kurusha mizinga na roketi dhidi ya maeneo lengwa ya baharini.
“PLA haitasita kamwe kuchukua hatua dhidi ya nguvu za mafarakano ya kutaka 'Taiwan Ijitenge' na kuhimiza muungano wa taifa. Itaendelea kutekeleza operesheni za kukabiliana na kujitenga na uingiliaji wa nje, kulinda kithabiti mamlaka, umoja, na ukamilifu wa ardhi ya China”, amesema Zhang Xiaogang, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



