Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa China, Cambodia na Thailand wafikia makubaliano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 30, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), pamoja na Prak Sokhonn, Naibu Waziri Mkuu wa Cambodia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na Sihasak Phuangketkeow, Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand, wakihudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa China, Cambodia na Thailand mjini Yuxi, Mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China, Desemba 29, 2025. (Xinhua/Wang Guansen)

KUNMING - Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa China, Cambodia na Thailand umefanyika kwa mafanikio Jumatatu mjini Yuxi, Mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China.

Kufuatia kusainiwa kwa taarifa ya pamoja kuhusu kusimamisha mapigano, mawaziri wa mambo ya nje wa Cambodia na Thailand waliongoza ujumbe wao kukutana mkoani Yunnan, China kuanzia Desemba 28 hadi 29 kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi.

"Tangu kuzuka kwa mgogoro kwenye mpaka kati ya Cambodia na Thailand, China imekuwa ikishiriki katika upatanishi," Wang amesema, akiongeza kuwa China kwa mara nne imemtuma mjumbe wake maalum wa masuala ya Asia kufanya diplomasia ya upatanishi kati ya pande hizo mbili, ili kushughulikia maslahi halali ya kila upande na kutafuta suluhu kupitia mazungumzo na majadiliano.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kwamba China inafurahi kuona kwamba Cambodia na Thailand zimefikia makubaliano ya hivi karibuni ya kusimamisha mapigano.

Wang amesema mamlaka za mambo ya nje na za kijeshi za Cambodia na Thailand zimekuwa na mazungumzo ya kina kuhusu suala hilo, na pande zote mbili zimeonyesha dhamira ya kupunguza mvutano na kuimarisha uhusiano wa pande mbili kwa msingi wa kusimamisha mapigano.

Wang ameongeza kuwa majadiliano kati ya pande hizo tatu yamekuwa ya kiujenzi na yenye matokeo, na kusababisha makubaliano muhimu yafuatayo:

Kwanza, pande zote zinapaswa kutazama mbele na kusonga mbele pamoja. Pili, maendeleo yanapaswa kufanyika hatua kwa hatua na kuepuka kusimama. Tatu, kujenga upya hali ya kuaminiana ni kipaumbele.

Wang amesema kwamba China itasaidia kuimarisha uhusiano kati ya Cambodia na Thailand, na inapenda kutoa msaada unaohitajika, ikiwemo ufuatiliaji wa usimamishaji mapigano, misaada ya kibinadamu na ushirikiano wa kutegua na kuondoa mabomu ya ardhini.

Kwa upande wao, mawaziri wa mambo ya nje wa Cambodia na Thailand wameishukuru China kwa kutoa jukwaa hilo la mazungumzo, na wamesifu jukumu la kiujenzi la China katika kupunguza mgogoro, kurudisha utulivu, na kuhimiza mazungumzo.

Pande zote mbili zimesisitiza thamani ya amani, na zimeonyesha utayari wa kutekeleza makubaliano hayo ya kusimamisha mapigano, kutumia vyema mifumo ya mazungumzo katika ngazi mbalimbali kushughulikia tofauti, na kufanya kazi pamoja kulinda amani na utulivu kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Prak Sokhonn, Naibu Waziri Mkuu wa Cambodia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na Sihasak Phuangketkeow, Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand wakihudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa China, Cambodia na Thailand mjini Yuxi, Mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China, Desemba 29, 2025. (Xinhua/Wang Guansen)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha