Trump atishia shambulizi jipya dhidi ya Iran kama itajaribu kujenga upya mpango wa silaha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 30, 2025

Picha iliyopigwa kutoka kwenye video iliyotolewa na Ikulu ya White House ikimwonesha Rais wa Marekani Donald Trump akikutana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kwenye eneo la Mar-a-Lago huko Palm Beach, Florida, Marekani, Desemba 29, 2025. (Xinhua)

Picha iliyopigwa kutoka kwenye video iliyotolewa na Ikulu ya White House ikimwonesha Rais wa Marekani Donald Trump akikutana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kwenye eneo la Mar-a-Lago huko Palm Beach, Florida, Marekani, Desemba 29, 2025. (Xinhua)

WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kwamba kama Tehran itajaribu kujenga upya mpango wa silaha, Marekani itaanzisha shambulizi mara nyingine tena dhidi ya Iran.

"Sasa nasikia kwamba Iran inajaribu kujenga tena zana za silaha, na kama wanafanya hivyo, inatubidi tuzipige na kuzibomoa", Trump amewaambia waandishi wa habari jana Jumatatu wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu huko Florida.

"Tutazipiga ili kuzibomoa. Tutaziteketeza kabisa” amesema, akiongeza kwamba kufikia "makubaliano" ni "chaguo bora zaidi" kwa Iran.

Mapema mwezi huu, Shirika la Habari la NBC liliripoti kwamba wakati wa mazungumzo yao hayo ya Jumatatu, Netanyahu atakuwa akitafuta kumshawishi Trump kwamba "upanuzi wa Iran wa mpango wake wa makombora ya balestiki unaleta tishio ambalo linaweza kuhitaji hatua za haraka."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, alisema wiki iliyopita kwamba mpango wa makombora wa Iran ni kwa ajili ya kulinda mamlaka ya nchi hiyo na ni "usiojadilika."

Tarehe 13 ya Mwezi Juni mwaka huu, Israeli ilianzisha mashambulizi ya ghafla dhidi ya maeneo kadha wa kadha nchini Iran, ikiwa ni pamoja na majengo ya nyuklia na ya majengo ya kijeshi, na kusababisha vifo vya makamanda waandamizi, wanasayansi wa nyuklia, na raia. Juni 22, vikosi vya Marekani vilipiga kwa makombora vituo vitatu vya nyuklia vya Iran vya Natanz, Fordow na Isfahan.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha