Rais Xi Jinping atoa wito wa kusukuma mbele ustawi wa vijiji kwa pande zote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 31, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa kusukuma mbele ustawi wa vijiji kwa pande zote na kuhimiza maendeleo ya mafungamano kati ya miji na vijiji, na kuweka mkazo zaidi katika ujenzi wa mambo ya kisasa katika kilimo na vijiji.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo katika maagizo yake kuhusu kazi za kilimo, vijiji na wakulima, ambazo zilijadiliwa kwenye mkutano wa mwaka wa kamati kuu ya kazi za vijiji uliofanyika Beijing kuanzia Jumatatu hadi Jumanne wiki hii.

Mkutano huo ulichambua hali ya hivi sasa na changamoto zinazokabili kazi za vijiji za China na kupanga sera muhimu katika mwaka 2026.

Kabla ya mkutano huo, mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ulitoa maagizo kwa mkutano husika na kazi zinazohusu kilimo, vijiji na wakulima.

Rais Xi amesema, mwaka 2026 ni mwanzo wa kipindi cha utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano (2026-2030), na ni muhimu mkubwa sana kwa kufanya vizuri kazi zinazohusu kilimo, vijiji na wakulima.

"Jitihada zinapaswa kufanywa ili kuhakikisha uzalishaji wa nafaka na kuongeza matokeo mazuri ya sera za kuimarisha kilimo, kunufaisha maeneo ya vijijini, na kuwatajirisha wakulima," Rais Xi amesema.

Amesema China inapaswa kufanya juhudi za kuweka bei za nafaka na mazao mengine muhimu ya kilimo kwenye kiwango kinachofaa na kuhimiza mapato ya wakulima kuongezwa kwa hatua madhubuti.

Rais Xi ametoa wito wa kuimarisha na kupanua mafanikio katika kupunguza umaskini, na kuzuia wakazi wengi wa vijijini kurudi kwa mara nyingne tena kwenye hali ya umaskini.

"Ni lazima kuchukua hatua za kufuata hali halisi ya maeneo husika, na kujenga maeneo ya vijijini yawe ya kupendeza yenye hali ya maafikiano, ambayo yanafaa kuishi na kufanya kazi," amesema.

Rais Xi amesema China inapaswa kujitahidi kukijenga kilimo kuwa sekta muhimu zaidi ya kisasa na kufikia kimsingi vigezo vya maisha ya kisasa katika maeneo ya vijijini, na kuwawezesha wakulima kufurahia maisha yenye ustawi zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha