Uchomeleaji wa njia kuu wakamilika kwa mradi wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki unaojengwa na China

(CRI Online) Desemba 31, 2025

Uchomeleaji wa kuunganisha Njia Kuu ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki unaojengwa na kampuni ya Uhandisi ya Mafuta ya China (CPP) umekamilika, ikiashiria hatua kubwa katika maendeleo ya moja ya miradi mikubwa ya kuvuka mpaka ya miundombinu ya nishati ya Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa na CPP Jumatatu wiki hii, hadi kufikia Desemba 28, uchomeleaji kuunganisha njia kuu ya bomba hilo yenye urefu wa kilomita 1,426 ulikuwa umekamilika.

Taarifa hiyo imesema, bomba hilo linapitia katika mazingira magumu na yenye changamoto, ikiwemo maeneo oevu, mito, maeneo ya milimani na ukanda tete wa ikolojia, hivyo kuleta mahitaji makubwa katika kupanga na ujenzi, ulinzi wa mazingira, na usimamizi wa mradi.

(Wahariri wa tovuti:Renato Lu)

Picha