Wang Yi: ushawishi wa kimataifa wa China, uwezo wake wa kuongoza maendeleo mpya na mvuto wake wa kimaadili vimeongezeka kwa kiasi kikubwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 31, 2025

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kwamba uhusiano kati ya China na nchi nyingine duniani unaendelezwa katika mwelekeo chanya zaidi, na ushawishi wake wa kimataifa, uwezo wake wa kuongoza maendeleo mapya na mvuto wake wa kimaadili vimeongezeka kwa kiasi kikubwa katika mwaka 2025.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameyasema hayo alipohutubia kongamano kuhusu hali ya kimataifa na uhusiano wa nje wa China mwaka 2025.

"Mwaka huu, chini ya uongozi thabiti wa Kamati Kuu ya CPC ambayo Komredi Xi Jinping akiwa kiini chake, China imeshikilia juu bendera ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, kufuata mwongozo wa kimkakati wa diplomasia ya mkuu wa nchi, kuunganisha kwa dhati nguvu zinazoendeleza maendeleo kote duniani, na kujumuisha juhudi zote za amani na maendeleo," Wang amesema.

Amesema kuwa China imekuwa nanga ya uthabiti katika dunia yenye misukosuko ambapo amani iko hatarini, nguzo kuu katika mazingira mapya ya kikanda yanayozunguka mipaka yake, na nguvu ya msingi inayofafanua mwelekeo wa utaratibu wa kimataifa unaobadilika.

"Pia imekuwa injini kuu katika kukabiliana na changamoto za maendeleo duniani, na nguvu thabiti katika kukabiliana na changamoto muhimu kuhusu haki na uadilifu wa kimataifa." ameongeza.

Kwa kutupia macho siku za baadaye, Wang amesema kwamba diplomasia ya China kama nchi kubwa yenye umaalum wa China inapaswa kuwa na mafanikio makubwa zaidi mwaka 2026.

Amesema kwamba China itatoa uungaji mkono wa kimkakati ulio imara zaidi kwa maendeleo na ustawi wa kitaifa, kufungua njia mpya katika kujenga aina mpya ya uhusiano kati ya nchi kubwa, kufanya juhudi zaidi katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja na nchi jirani, na kuimarisha ushirikiano wa Nchi za Kusini katika safari yao ya kuelekea kisasa.

"China itaongeza msukumo mkubwa zaidi kwenye ufunguaji mlango na ushirikiano wa kimataifa, kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuufanyia mageuzi na kuuboresha usimamizi wa dunia, na kuchukuka hatua kwa hisia thabiti ya dhamira na uwajibikaji katika kulinda maslahi yake ya kitaifa," Wang ameongeza. 

(Wahariri wa tovuti:Renato Lu)

Picha