Lugha Nyingine
Kutembelea Kufurahia Eneo Jipya la Xiong'an la China: Mji wa siku za baadaye unaoendeshwa na teknolojia
Eneo Jipya la Xiong'an, katika Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China na lililoko umbali wa kilomita takriban 120 kusini-magharibi mwa Beijing, linaibuka kwa kasi, likitumia teknolojia kuonesha sifa za namna mji wa kisasa unaweza kuwa.
Kwenye skrini kubwa katika Kituo cha Mambo ya Kompyuta cha Mjini cha Xiong'an, mitiririko ya data hutoa uungaji mkono wenye ufanisi wa mambo ya kompyuta kwa shughuli za mji, ikifanya kituo hicho kuwa kitovu cha kusambaza data mbalimbali kwa mji huo wa teknolojia fanisi za kisasa.
Eneo Jipya la Xiong'an ni mahali pa kwanza nchini China kuanzisha dhana ya "mji pacha wa kidijitali," amesema Zhang Xuexiang kutoka idara ya mfumo wa upashanaji habari katika Kampuni ya Teknolojia ya Xiong'an Cloud Network. Ameelezea kwamba kila jengo, barabara, na bomba katika ulimwengu halisia vina "pacha" wa kidijitali kwenye jukwaa la mtandao.
Ukiongozwa na Kituo hicho cha Mambo ya Kompyuta cha Mjini cha Xiong'an, mfumo wa usafiri wa eneo hilo unapitia mageuzi tulivu. Mitandao ya kidijitali ya barabara imejumuishwa kwa kina na magari yaliyounganishwa na AI, ikiunda mfumo wa mazingira ya usafiri ulioratibiwa ambapo "barabara fanisi za kisasa" na "magari yenye teknolojia fanisi za kisasa" hufanya kazi pamoja.
Je mustakabali unaonekana namna gani? Katika Eneo Jipya la Xiong'an, jibu tayari linaonekana.

Picha ikionyesha Kituo cha Mambo ya Kompyuta cha Mjini cha Xiong'an katika Eneo Jipya la Xiong'an, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China. (Picha kwa hisani ya ofisi ya masuala ya uenezi na mtandao wa anga ya Eneo Jipya la Xiong'an)

Mfanyakazi akifanya kazi mbele ya jukwaa la kidijitali kwenye Kituo cha Mambo ya Kompyuta cha Mjini cha Xiong'an katika Eneo Jipya la Xiong'an, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China. (People's Daily Online/Yuan Meng)

Roboti ya 5G ya barista ikitengeneza kahawa kwenye mkahawa ndani ya Kituo cha Kujionea na Kutumia Uvumbuzi wa Sayansi na Teknolojia cha Kampuni ya China Mobile katika Eneo Jipya la Xiong'an, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China. (People's Daily Online/Su Yingxiang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



