Timu ya madaktari wa China yatoa vitu vya msaada kwa watoto yatima wa Sierra Leone

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2026

Justina Zainab Conteh (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mtakatifu George, akikabidhi bamba la shukrani kwa Timu ya 26 ya Madaktari wa China nchini Sierra Leone katika Nyumba ya Ustawi wa Watoto ya Mfuko wa Mtakatifu George mjini Freetown, Sierra Leone, Januari 2, 2026. (Kundi la 26 la Timu ya Madaktari wa China nchini Sierra Leone/kupitia Xinhua)

FREETOWN - Timu ya 26 ya Madaktari wa China nchini Sierra Leone imetoa vitu vya msaada vikiwa ni zawadi za Mwaka Mpya kwa nyumba ya ustawi mjini Freetown, Sierra Leone.

Vitu hivyo vya msaada, vikiwemo mchele, mkate, vitafunio, na mahitaji ya kila siku, vimekabidhiwa kwa Nyumba ya Ustawi wa Watoto ya Mfuko wa Mtakatifu George siku ya Alhamisi ikiwa ni sehemu ya juhudi za timu hiyo za kuboresha afya na maisha ya kila siku ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini humo.

Wakati wa kutembelea nyumba hiyo ya watoto, Liu Longfei, mkuu wa timu hiyo ya madaktari, ameelezea matumaini kwa watoto hao, akisema watakuwa wapokeaji jukumu katika kuijenga Sierra Leone na warithi wa urafiki kati ya China na Sierra Leone.

Liu amesema timu hiyo ya madaktari imekuwa ikitoa huduma ya afya bila malipo kwa watoto kwa muda mrefu katika nyumba hiyo ya ustawi wa jamii kwa kutumia matibabu ya jadi ya China na kuleta vitu vya msaada ili kuboresha maisha yao.

Justina Zainab Conteh, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mtakatifu George, ameelezea shukrani zake kwa uungaji mkono huo wa timu ya madaktari wa China na serikali ya China.

Timu ya 16 ya Madaktari wa China nchini Sierra Leone wakipiga picha pamoja katika Nyumba ya Ustawi wa Watoto ya Mfuko wa Mtakatifu George mjini Freetown, Sierra Leone, Januari 1, 2026. (Kundi la 26 la Timu ya Madaktari wa China nchini Sierra Leone/kupitia Xinhua)

Timu ya 26 ya Madaktari wa China nchini Sierra Leone wakipiga picha ya kundi katika Nyumba ya Ustawi wa Watoto ya Mfuko wa Mtakatifu George mjini Freetown, Sierra Leone, Januari 1, 2026. (Kundi la 26 la Timu ya Madaktari wa China nchini Sierra Leone/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha