China yalaani vikali Marekani kutumia nguvu ya kijeshi dhidi ya Venezuela

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2026

BEIJING - China imeshtushwa sana na inalaani vikali Marekani kutumia waziwazi nguvu ya kijeshi dhidi ya nchi huru yenye mamlaka na kuchukua hatua dhidi ya rais wake, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema mjini Beijing jana Jumamosi.

Habari zimesema kwamba Marekani ilifanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Venezuela, na Rais wa Marekani Donald Trump alichapisha kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social kwamba Marekani "kwa mafanikio" imefanya shambulio kubwa dhidi ya Venezuela, na kiongozi wake, Rais Nicolas Maduro, pamoja na mkewe, wamechukuliwa na "kusafirishwa kwa ndege nje ya nchi."

Msemaji huyo amesema, vitendo vya namna hiyo vya kimwamba vya Marekani vinakiuka vibaya sheria ya kimataifa na mamlaka ya nchi ya Venezuela, na kutishia amani na usalama katika Latini Amerika na eneo la Karibian. Ameongeza kuwa, China inapinga vikali vitendo hivyo.

"Tunatoa wito wa kuitaka Marekani kufuata sheria za kimataifa na nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, na kuacha kukiuka mamlaka na usalama wa nchi nyingine," amesema msemaji huyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha