Rais Xi ampongeza Doumbouya kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Guinea

(CRI Online) Januari 05, 2026

Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za kumpongeza Mamady Doumbouya leo Jumatatu kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Guinea.

Katika ujumbe wake huo Rais Xi amesema kwamba Guinea ni nchi ya kwanza katika Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China.

Amesema kwa muda mrefu, pande hizo mbili zimekuwa zikifuata kanuni za kuheshimiana, usawa, na kunufaishana, zikiungana mkono katika masuala yanayohusu maslahi yao ya msingi na masuala muhimu, na kufanya ushirikiano wenye kuzaa matunda katika kutafuta maendeleo ya pamoja.

Ameeleza kutilia mkazo maendeleo ya uhusiano kati ya China na Guinea, na kwamba yuko tayari kufanya kazi na Rais Doumbouya ili kuhimiza maendeleo makubwa ya uhusiano wa kiwenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya ustawi wa watu wa nchi hizo mbili na mshikamano wa Nchi za Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha