China yarekodi safari milioni 142 za kwenda kufanya utalii wa ndani wakati wa likizo ya Mwaka Mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 05, 2026

Picha iliyopigwa Januari 3, 2026 ikionyesha watalii wakitembelea eneo la vivutio vya utalii la Hekalu la Confucius mjini Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. (Picha na Liu Jianhua/Xinhua)

Picha iliyopigwa Januari 3, 2026 ikionyesha watalii wakitembelea eneo la vivutio vya utalii la Hekalu la Confucius mjini Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. (Picha na Liu Jianhua/Xinhua)

BEIJING – Takwimu rasmi zilizotolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China jana Jumapili zinaonesha kuwa jumla ya safari za utalii wa ndani zimefikia milioni 142 katika mapumziko ya siku tatu ya Mwaka Mpya, ambapo matumizi ya jumla ya utalii yamefikia yuan karibu bilioni 84.8 (dola za Marekani takribani bilioni 12.1).

Wizara hiyo imeeleza kuwa maeneo ya mandhari ya majira ya baridi, maeneo yenye mwanga wa jua na safari za utalii wa masafa mafupi zimekaribishwa zaidi na watalii wakati wa mapumziko hayo, na hayo yote yameonesha matumizi bado ni yenye nguvu hai ya kutosha nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha