Lugha Nyingine
Mahakama ya Juu ya Guinea yathibitisha ushindi wa Mamady Doumbouya katika uchaguzi wa rais
Mahakama ya Juu ya Guinea jana Jumapili jioni imethibitisha rasmi matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 28 Desemba, na kumtangaza Bw. Mamady Doumbouya kuwa mshindi kwa kupata asilimia 86.72 ya kura zote halali zilizopigwa na kuwa rais wa Guniea.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari, jaji kiongozi wa mahakama hiyo ya juu ya Guinea Bw. Fode Bangoura, ametangaza rasmi kuchaguliwa kwa Doumbouya kuwa rais kwa kipindi cha muda wa miaka saba kwa mujibu wa katiba ya Guinea.
Uchaguzi huo wa urais unaashiria hatua muhimu katika juhudi za Guinea za kurejesha utulivu wa kikatiba.
Mwezi Septemba mwaka 2021 rais wa wakati huo Alpha Conde aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi, baadaye serikali ya mpito iliyoongozwa na Bw. Doumbouya ilichukua madaraka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



