Lugha Nyingine
Rais wa Nigeria awabaini magaidi wanaohusika na mauaji na utekaji katika Jimbo la Niger
Rais Bola Tinubu wa Nigeria amesema wahusika wa raundi ya hivi karibuni ya mashambulizi, ambayo yameua watu zaidi ya 30 na kushuhudia makumi ya watu wakitekwa nyara kwenye soko la kijiji cha Demo katika Jimbo la Niger ni wanaodhaniwa kuwa magaidi waliokimbia mashambulizi ya anga dhidi yao yaliyofanywa na Marekani katika maeneo ya Sokoto na Zamfara.
Katika taarifa iliyotolewa jana Jumapili na Msemaji wa rais huyo, Bayo Onanuga, Rais Tinubu ameagiza mamlaka za usalama kuwasaka na kuwakamata watu waliohusika na shambulizi hilo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria, huku akitaka mamlaka hizo kuwaokoa mateka wote.
Kwa mujibu wa msemaji wa Polisi wa jimbo hilo la Niger, Wasiu Abiodun, magaidi hao waliingia kwenye kijiji hicho kupitia Mbuga ya Msitu wa Taifa iliyoko katika eneo hilo na kufanya uharibifu mkubwa ikiwemo kuchoma moto maduka na kupora chakula.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



