Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na mwenzake wa Korea Kusini Lee Jae Myung, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 5, 2026. (Xinhua/Liu Bin)
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na Rais Lee Jae Myung wa Korea Kusini mjini Beijing jana Jumatatu ambapo amesema yeye na Rais Lee wamekutana mara mbili na kufanya ziara katika nchi hizo mbili, ikionyesha umuhimu mkubwa ambao pande zote mbili zinautambua katika uhusiano kati ya China na Korea Kusini.
Amesema kwa kuwa zote ni marafiki na majirani, China na Korea Kusini zinapaswa kuongeza mawasiliano na kudumisha mawasiliano ya mara kwa mara.
"China kwa muda mrefu imekuwa ikiweka uhusiano na Korea Kusini katika nafasi ya juu kwenye ajenda yake ya diplomasia ya kikanda na kudumisha mwendelezo na utulivu wa sera zake kuhusu Korea Kusini," Rais Xi amesema, akiongeza kuwa China ina nia ya kushirikiana na Korea Kusini ili kushikilia kwa uthabiti mwelekeo wa ushirikiano wa kirafiki, kuzingatia kanuni ya kunufaishana, kuhimiza ushirikiano wa kimkakati wa pande mbili kwenye njia nzuri, kuboresha kwa vitendo ustawi wa watu wa pande zote mbili, na kutoa mchango vyema kwa amani na maendeleo ya kikanda na kimataifa.
Rais Xi amesisitiza kwamba China na Korea Kusini kwa muda mrefu zimekuwa zikifuata kanuni za kuthamini amani juu ya yote na kutetea mapatano pasipo ufanano, kanuni ambazo zimevuka tofauti za mifumo ya kijamii na itikadi, na kuwezesha nchi hizo kusaidiana kufanikiwa na kupata maendeleo kwa pamoja.
Rais Xi ametoa wito kwa pande zote mbili kuendeleza desturi hiyo nzuri, kuimarisha hali ya kuaminiana, kuheshimu njia za maendeleo za kila upande, kuzingatia maslahi ya msingi na masuala makuu yanayofuatiliwa na kila upande, na kushughulikia tofauti ipasavyo kupitia mazungumzo na mashauriano.
"China na Korea Kusini zinabeba majukumu muhimu katika kudumisha amani ya kikanda na kuhimiza maendeleo ya dunia, na zina maslahi mengi ya pamoja," Rais Xi amesema, akieleza kuwa nchi hizo mbili zinapaswa kusimama kithabiti kwenye upande sahihi wa historia na kufanya maamuzi sahihi ya kimkakati.
Kwa upande wake, Rais Lee amesema Korea Kusini na China ni majirani wa karibu wenye uhusiano wa muda mrefu, akibainisha kuwa nchi hizo mbili zilipambana bega kwa bega dhidi ya uvamizi wa kijeshi wa Japan, na kwamba upande wa Korea Kusini unashukuru juhudi za China katika kuhifadhi maeneo ya kihistoria ya harakati za uhuru wa Korea nchini China.
"Tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, nchi hizo mbili zimejenga uhusiano wa karibu wa ushirikiano na kufikia mafanikio yenye matunda," Rais Lee amesema, akiongeza kuwa Korea Kusini inaupa umuhimu mkubwa sana uhusiano wake na China.
Amesisitiza kwamba Korea Kusini inaheshimu maslahi ya kimsingi na masuala makuu yanayofuatiliwa ya China, na inafuata kanuni ya kuwepo kwa China moja.
Baada ya mazungumzo yao, Marais hao wawili walishuhudia kusainiwa kwa nyaraka 15 za ushirikiano katika nyanja zikiwemo uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, mazingira ya ikolojia, usafirishaji, na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara.
Kabla ya mazungumzo hayo, Rais Xi na mkewe, Peng Liyuan, walifanya hafla ya kuwakaribisha Rais Lee na mkewe, Kim Hea Kyung, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma.

Rais Xi Jinping wa China na Rais Lee Jae Myung wa Korea Kusini wakishuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano baada ya mazungumzo yao mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 5, 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)

Rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan wakipiga picha ya pamoja na Rais Lee Jae Myung wa Korea Kusini na mkewe Kim Hea Kyung mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 5, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais Lee Jae Myung wa Korea Kusini kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 5, 2026. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais Lee Jae Myung wa Korea Kusini kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 5, 2026. (Xinhua/Shen Hong)

Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Rais Lee Jae Myung wa Korea Kusini kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 5, 2026. (Xinhua/Xie Huanchi)

Misri yashuhudia idadi inayovunja rekodi ya watalii milioni 19 katika mwaka 2025

Handaki refu zaidi duniani la barabara ya mwendokasi lakamilika

Ndege wa kuhamahama waonekana katika Ziwa Donggu mkoani Hunan, katikati mwa China

Jukwaa jipya la kutazamia mandhari laonyesha mandhari ya mji wa Tianjin, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma