China yatoa stempu za Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi na kuchochea shauku zaidi ya wakusanyaji stempu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 06, 2026

Mfanyakazi akionyesha stempu maalum  za ukumbusho wa Mwaka Mpya wa Farasi wa Jadi mjini Anqing, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Januari 5, 2026. (Picha na Xu Huoju/Xinhua)

Mfanyakazi akionyesha stempu maalum za ukumbusho wa Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi mjini Anqing, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Januari 5, 2026. (Picha na Xu Huoju/Xinhua)

BEIJING – Shirika la Posta la China limetoa rasmi seti ya stempu maalum jana Jumatatu katika kusherehekea Mwaka Mpya wa jadi wa Farasi unaowadia, na kuleta msisimko mkubwa miongoni mwa wanunuzi wa kukusanya stempu za ukumbusho.

Ingawa hali ya hewa ilikuwa baridi kali, foleni ndefu zilianza kujitokeza kwenye ofisi za posta katika maeneo mbalimbali mjini Beijing mapema juzi Jumapili alasiri. Kufikia saa 2 asubuhi jana Jumatatu, mauzo yalipoanza rasmi, wanunuzi wenye shauku ya kukusanya stempu za ukumbusho -- kuanzia mashabiki wa kila majira wa stempu hadi wapenzi wanaochipukia -- walikuwa tayari wamejipanga kando ya njia za watembea kwa miguu.

Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi utawadia Februari 17, 2026 kwa kalenda ya kilimo ya China. Sherehe za mwaka huu zinabeba umuhimu zaidi wa kiutamaduni kufuatia kuorodheshwa kwa mafanikio mila na desturi za jamii za kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwenye Orodha ya Uwakilishi ya UNESCO ya Mali za Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Binadamu mwaka 2024, tukio muhimu ambalo limeongeza shauku ya umma juu ya mila na desturi za jadi.

Seti ya stempu hizo maalumu ina stempu mbili zenye thamani ya jumla ya yuan 2.40 (senti za Marekani karibu 34).

Stempu ya kwanza inaonyesha farasi mwekundu akitembea kukanyaga mawingu, ikiashiria maendeleo tulivu ya uchumi na jamii na kuonyesha matarajio ya taifa kuelekea malengo ya baadaye ya Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya Miaka Mitano (2026-2030). Stempu ya pili inaonesha farasi watatu wanaokimbia wakiwa kwenye michoro ya baraka na neema, ikionesha watu wa makabila yote wa China wanashikamana na kufanya juhudi za pamoja katika kujenga nchi ya mambo ya kisasa ya kijamaa na kusukuma mbele ustawishaji mkubwa wa Taifa la China kwa pande zote.

Katika utamaduni wa China, farasi ni alama ya uhai, nguvu, na mafanikio. Mara nyingi akihusishwa na nahau "Ma Dao Cheng Gong" -- inayomaanisha "mafanikio ya papo hapo mara tu farasi anapowasili" -- mnyama huyo anawakilisha moyo wa uthabiti na uvumilivu na maendeleo ya haraka.

Farasi kwa muda mrefu wanathaminiwa kwa kazi zao katika usafirishaji na ustawi, na hivi leo bado ni alama inayopendwa zaidi katika kalenda ya kilimo ya China, ambayo wanyama 12 ambao kila mnyama anawakilisha mwaka mmoja kwa mzunguko wa miaka 12, na uwakilishi wa Farasi umechukuliwa kuwa ni alama ya nishati na maendeleo katika mwaka mpya.

"Si tu ni mafanikio katika usanifu bali pia ni uzoefu ulivyo wa kunufaika na maendeleo ya utamaduni pamoja na watu," amesema Liu Aili, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Kundi la Posta la China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha