Maduro Akana Hatia kwa Mashtaka Mahakamani nchini Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 06, 2026

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha watu wakiandamana nje ya mahakama mjini New York, Marekani, Januari 5, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

NEW YORK - Rais wa Venezuela Nicolas Maduro jana Jumatatu alikana hatia kwa mashtaka yote ya Marekani wakati wa kufikishwa kwake mahakamani kwa mara ya kwanza mjini New York.

"Sina hatia, sina kosa," Maduro amesema mahakamani, akiongeza kwamba "alitekwa nyara" nyumbani kwake huko Caracas, na angali bado ni rais wa Venezuela, vyombo vya habari vimeripoti ndani ya mahakama.

Mke wa Maduro, Cilia Flores, amesema mahakamani kwamba hana hatia kabisa kwa mashtaka yaliyoletwa na Marekani dhidi yake.

Tarehe ijayo ya kusikilizwa kwa kesi hiyo dhidi ya Maduro imepangwa kuwa Machi 17.

Waandamanaji waliokusanyika nje ya mahakama walikuwa wakipiga kelele za upingaji na kushikilia mabango ya "Mwachie Huru Maduro" "Acha Vita dhidi ya Venezuela," na "Marekani ondoa mikono kwa Venezuela."

"Mashtaka haya ni ya kushtusha kabisa," Sydney Loving, mmoja wa waandamanaji ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua. "Tunapinga aina yoyote ya uingiliaji kama huo kwa nchi yenye mamlaka."

"Kumteka nyara rais wa nchi nyingine ni kuvuka mstari mwekundu kabisa. Hakika inakiuka sheria za kimataifa," amesema.

Asubuhi mapema ya Jumamosi iliyopita, vikosi vya Jeshi la Marekani vilifanya mashambulizi na kurusha makombora dhidi ya Caracas na sehemu nyingine za Venezuela na kuwachukua Maduro na mkewe kwa nguvu, na baadaye kuwaweka kizuizini New York.

Mashambulizi hayo ya Marekani yameishtua jumuiya ya kimataifa, na kusababisha mfululizo wa lawama na ufuatiliaji mkubwa duniani kote.

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha watu wakiandamana nje ya mahakama mjini New York, Marekani, Januari 5, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha watu wakiandamana nje ya mahakama mjini New York, Marekani, Januari 5, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha mwonekano wa nje ya mahakama, ambapo Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amepelekwa kushtakiwa, New York, Marekani, Januari 5, 2026. (Xinhua/Zhang Fengguo)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha