Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa: hatua za kijeshi za Marekani dhidi ya Venezuela hazikuheshimu sheria za kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 06, 2026

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kisiasa Rosemary DiCarlo (kati, mbele) akizungumza katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Januari 5, 2026. (Loey Felipe/Picha ya Umoja wa Mataifa/kupitia Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonyesha wasiwasi wake mkubwa kuhusu kutoheshimiwa kwa sheria za kimataifa katika hatua za kijeshi za Marekani dhidi ya Venezuela siku ya Jumamosi.

"Ninaendelea kuwa na wasiwasi mkubwa kwamba kanuni za sheria za kimataifa hazikuheshimiwa kuhusiana na hatua za kijeshi za Januari 3," Guterres amesema jana Jumatatu katika taarifa kwa Baraza la Usalama, iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu wa Masuala ya Siasa Rosemary DiCarlo.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa Katiba ya Umoja wa Mataifa unaweka marufuku ya tishio au matumizi ya nguvu dhidi ya ukamilifu wa ardhi au uhuru wa kisiasa wa nchi yoyote.

"Kudumisha amani na usalama wa kimataifa kunategemea nchi zote wanachama (wa Umoja wa Mataifa) kuendelea kufuata vifungu vyote vya katiba hiyo," amesema Guterres.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia ameonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa hali ya ukosefu wa utulivu nchini Venezuela, athari zake kwa kanda, na mfano mbaya ambao operesheni ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela inaweza kuweka katika uendeshaji wa uhusiano kati ya nchi.

Ametoa wito kwa wadau wote wa Venezuela kushiriki katika mazungumzo jumuishi na ya kidemokrasia, ambapo sekta zote za jamii zinaweza kuamua mustakabali wao, na akazisihi nchi jirani wa Venezuela, na jumuiya ya kimataifa kwa upana zaidi kuchukua hatua kwa moyo wa mshikamano na kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu zilizowekwa ili kuhimiza kuishi pamoja kwa amani.

"Nguvu ya sheria lazima idumishwe," amesema Guterres, akiongeza kuwa sheria ya kimataifa ina zana za kushughulikia masuala kama vile usafirishaji haramu wa dawa za kulevya, migogoro ya rasilimali na masuala ya haki za binadamu.

"Hii ndiyo njia tunayohitaji kuchukua," amesema. 

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Siasa Rosemary DiCarlo (mbele) akizungumza katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Januari 5, 2026. (Mark Garten/Picha ya Umoja wa Mataifa/kupitia Xinhua)

Balozi wa Somalia katika Umoja wa Mataifa Abukar Dahir Osman (mbele) akiongoza mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Januari 5, 2026. (Mark Garten/Picha ya Umoja wa Mataifa/kupitia Xinhua)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mkutano wa dharura kuhusu Venezuela kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Januari 5, 2026. (Loey Felipe/Picha ya Umoja wa Mataifa/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha