UNICEF yakabidhi vyandarua kwa Sudan Kusini kuunga mkono uzuiaji wa malaria

(CRI Online) Januari 06, 2026

Shirika la Mfumo wa Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limekabidhi shehena ya kwanza kati ya jumla ya vyandarua milioni 9.5 vya kuua na kufukuza mbu vyenye kudumu kwa muda mrefu ili kuunga mkono kampeni ijayo ya Sudani Kusini ya kuzuia maambukizi ya malaria.

Naibu Mwakilishi wa UNICEF nchini Sudan Kusini Ismali Kamil amesema vyandarua hivyo vimechangiwa na shirika la hisani linalojulikana kwa jina la “Against Malaria Foundation”, na vimesafirishwa hadi nchini humo na UNICEF, kwa uungaji mkono wa washirika wa maendeleo.

“Hadi kufikia leo, tumeshapokea vyandarua 763,000 vilivyosafirishwa katika makontena 20, ambavyo tayari vimewasili Juba. Shehena zingine, zilizosalia ziko bado njiani na zitawasili kwa awamu kuhakikisha maandalizi rahisi na yasiyosimama ya kampeni” Kamil amesema.

Ameongeza kuwa kampeni hiyo ya utoaji wa vyandarua kwa wingi inalenga kuhakikisha kila familia nchini Sudan Kusini inaweza kuwa na ufikiaji wa chandarua cha mbu, kulingana na kiwango cha kitaifa cha chandarua kimoja kwa kila watu 1.5.

Amesema kampeni hiyo inalenga kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi, ugonjwa, na vifo vinavyotokana na malaria, hasa miongoni mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 na akina mama wajawazito.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha