Lugha Nyingine
Idadi ya waliokufa kwenye ajali ya boti nchini Nigeria yaongezeka hadi 29
Shirika la Usimamizi wa Dharura la Jimbo la Yobe nchini Nigeria limesema jana Jumatatu kuwa idadi ya vifo kutokana na ajali ya boti iliyotokea katika Jimbo hilo la kaskazini mwa Nigeria imeongezeka kutoka 25 hadi 29.
Mkuu wa shirika hilo Bw. Mohammed Goje, amewaambia wanahabari huko Damaturu, mji mkuu wa jimbo hilo kuwa wahudumu wa mambo ya dharura na wakazi wenyeji wa kujitolea waliopoa miili minne zaidi kutoka Mto Yobe siku hiyo ya Jumatatu.
Bw. Goje amesema takriban watu wanane hadi 10 zaidi bado hawajulikani walipo, akibainisha kuwa operesheni ya uokoaji imeimarishwa ili kuokoa waathirika zaidi.
Ajali hiyo ilitokea baada ya boti ya mbao iliyokuwa imebeba abiria 52, wengi wao wakiwa wavuvi na wakulima wenyeji, kuzama kwenye Mto Yobe siku ya Jumamosi usiku.

Misri yashuhudia idadi inayovunja rekodi ya watalii milioni 19 katika mwaka 2025

Handaki refu zaidi duniani la barabara ya mwendokasi lakamilika

Ndege wa kuhamahama waonekana katika Ziwa Donggu mkoani Hunan, katikati mwa China

Jukwaa jipya la kutazamia mandhari laonyesha mandhari ya mji wa Tianjin, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma