Muda wa nyongeza waipeleka Algeria robo fainali huku Mabingwa watetezi Côte d'Ivoire nao wakifuzu

(CRI Online) Januari 07, 2026

Mchezaji Adil Boulbina aliutumia vizuri muda wa nyongeza kwa kuipatia bao Algeria dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kuipeleka nchi hiyo katika hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mwaka 2025 (AFCON) yanayoendelea nchini Morocco.

Mchezo huo uliokuwa mgumu uliilazimu Algeria kusubiri hadi muda wa nyongeza ili kuondoka na ushindi wa 1-0 dhidi ya DRC mjini Rabat Morocco.

Nao mabingwa watetezi Côte d'Ivoire, kiu yao ya kupata mataji mfululizo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) iliongezeka siku hiyo ya Jumanne usiku huko Marrakesh, baada ya kuibamiza Burkina Faso kwa 3-0 na kufuzu katika hatua ya robo fainali ya AFCON.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha