Ghasia zinazozidi kuongezeka jimboni Ituri DRC zazuia operesheni za kibinadamu

(CRI Online) Januari 07, 2026

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeonya kuwa kuongezeka kwa ghasia katika Jimbo la Ituri, nchini DRC kumeathiri sana operesheni za uokoaji wa maisha katika eneo hilo.

Bw. Dujarric amesema mji wa Bule na maeneo jirani yameendelea kukumbwa na uhasama tangu mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka uliopita, na mamlaka za huko zimeripoti kuwa raia zaidi ya 25 wameuawa na zaidi ya 40 kujeruhiwa katika mwezi uliopita.

Bw. Dujarric ameongeza kuwa ripoti hiyo ya OCHA inaonesha kuwa ghasia hizo zimesababisha kukatizwa kwa msaada kwa watu zaidi ya 87,000 waliokimbia makazi yao, na kwamba familia hizo zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, huduma za afya na maji safi.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha