Waziri wa Mambo ya Nje wa China kufanya ziara katika nchi za Ethiopia, Somalia, Tanzania na Lesotho

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 07, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi atafanya ziara katika nchi za Ethiopia, Somalia, Tanzania na Lesoto kuanzia Januari 7 hadi 12, kwa mwaliko wa pande husika.

Kwa mujibu wa tangazo lilotolewa leo Jumtano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) wakati wa ziara hiyo barani Afrika pia atahudhuria hafla ya ufunguzi wa "Mwaka wa Mawasiliano ya kati ya Watu wa China na Afrika" kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Hii inatimiza mwaka wa 36 mfululizo ambapo Waziri wa Mambo ya Nje wa China ameifanya Afrika kuwa sehemu ya ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi ya mwaka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha