Kiasi cha mizigo cha ushoroba mkubwa wa biashara wa China chafikia rekodi ya juu mwaka 2025

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 07, 2026

Picha iliyopigwa Desemba 29, 2025 ikionyesha treni ya kwanza ya mizigo kutoka Mji wa Fangchenggang katika Mkoa wa Guangxi hadi Eneo la Qijiang la Mji wa Chongqing ikiwasili kwenye kituo cha reli cha Qijiang Kaskazini katika Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Chen Cheng)

Picha iliyopigwa Desemba 29, 2025 ikionyesha treni ya kwanza ya mizigo kutoka Mji wa Fangchenggang katika Mkoa wa Guangxi hadi Eneo la Qijiang la Mji wa Chongqing ikiwasili kwenye kituo cha reli cha Qijiang Kaskazini katika Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China. (Xinhua/Chen Cheng)

NANNING - Huduma ya reli ya Ushoroba Mpya wa Biashara ya Kimataifa wa Nchi kavu na Baharini wa China imeshughulikia jumla ya makontena milioni 1.425 (TEUs) mwaka 2025, kiwango cha juu kabisa kuwahi kufikia, ikiwa ni ongezeko la asilimia 47.6 na kuvuka idadi ya makontena milioni moja kwa mara ya kwanza, Shirika la Reli la China Tawi la Nanning limesema jana Jumanne.

Shirika hilo limesema kwamba kati ya jumla hiyo, makontena 701,000 yalisafirishwa kutoka maeneo ya magharibi mwa China kama vile Sichuan, Chongqing, na Yunnan hadi bandari za kusini mwa China zikiwemo Bandari ya Ghuba ya Beibu na Bandari ya Zhanjiang, ikiwa ni ongezeko la asilimia 40.4. Wakati huohuo, makontena 724,000 yalisafirishwa kutoka bandari mbalimbali kwenda maeneo ya ndani ya magharibi mwa China, ikiwa ni ongezeko la asilimia 55.3.

Ili kuongeza uwezo wa ushindani, shirika hilo lilipanua orodha yake ya aina za mizigo zilizoidhinishwa kwa usafirishaji wa makontena hadi zaidi ya bidhaa 11,000, ikijumuisha karibu bidhaa zote zinazofaa kusafirishwa kwa makontena. Aidha, idadi ya njia za treni zenye ratiba maalum iliongezwa hadi 44, ikiwa ni ongezeko la 21 ikilinganishwa na mwishoni mwa mwaka 2024.

Ushoroba huo sasa unaunganishwa vizuri na Reli ya Usafirishaji wa Haraka ya mizigo ya China na Ulaya na treni za mizigo za China na Asia ya Kati, ikiwezesha huduma za mara kwa mara za njia kama vile "Bandari ya Ghuba ya Beibu-Chengdu-Poland/Ujerumani" kwa bidhaa za jumla, "Hainan-Qinzhou-Xi'an" kwa nafaka na mafuta, na "UAE-Qinzhou-Lanzhou" kwa magari, na kuunda mtandao wa kimataifa wa usafirishaji wenye ufanisi.

Ushoroba huo unaunganisha Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri upande wa kaskazini na Njia ya Hariri ya Baharini ya Karne ya 21 upande wa kusini, ukiratibiwa na Ukanda wa Kiuchumi wa Mto Yangtze na kuchukua jukumu muhimu katika mkakati wa maendeleo ya kikanda yaliyoratibiwa wa China.

Kwa mujibu wa shirika hilo, tangu kuanza kufanya kazi kwa majaribio mwaka 2017, ushoroba huo umeendelea kukua na kuwa njia ya kimkakati inayounganisha maeneo ya ndani ya China na masoko ya nchi za ASEAN pamoja na maeneo mengine duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha