Rais wa Mexico akataa Marekani kuingilia kati nchini humo kupambana na magenge ya dawa za kulevya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 07, 2026

Rais Claudia Sheinbaum wa Mexico akihudhuria mkutano na waandishi wa habari huko Mexico City, mji mkuu wa Mexico, Januari 5, 2026. (Picha na Francisco Canedo/Xinhua)

MEXICO CITY - Rais Claudia Sheinbaum wa Mexico amekataa uwezekano wa Marekani kuingilia kati nchini Mexico kwa lengo la kupambana na magenge ya dawa za kulevya, akisisitiza umuhimu wa kulinda mamlaka huru ya kitaifa na kuimarisha umoja wa nchi.

Kwenye mkutano wake wa kila siku na waandishi wa habari Jumatatu wiki hii, Rais Sheinbaum ametupilia mbali haja ya kufanya mazungumzo na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye mara kwa mara amependekeza kupeleka wanajeshi wa Marekani nchini Mexico kupambana na magendo ya dawa za kulevya.

Amesisitiza kwamba ushirikiano wowote wa kiusalama lazima ujengwe juu ya kuheshimiana, kuheshimu mamlaka huru ya kitaifa, na ushirikiano usio na utii kwa upande mwingine.

"Siamini katika uvamizi, hata sidhani kama ni jambo ambalo wanalichukulia kwa uzito mkubwa," amesema, akiongeza kuwa Trump mara kwa mara amesisitiza kwamba jeshi la Marekani linaweza kuingia katika ardhi ya Mexico, lakini akasema kuwa utawala wake "umesema hapana kwa msimamo thabiti."

"Tatizo la magendo ya dawa za kulevya haliwezi kutatuliwa kupitia hatua za kijeshi za kigeni," amesema Rais Sheinbaum, akiongeza kuwa serikali ya Mexico inatekeleza mkakati mpana wa kupambana na dawa za kulevya juu ya msingi wa kuimarisha taasisi za usalama wa taifa na kushughulikia masuala ya kijamii.

Amesisitiza kwamba usafirishaji haramu wa silaha kutoka Marekani hadi Mexico ni moja ya sababu kuu za uhalifu wa kikatili nchini humo.

Hata hivyo, serikali yake imepiga hatua katika kupambana na ukatili, huku takwimu rasmi kuanzia Oktoba 2024 hadi Novemba 2025 zikionyesha kiwango cha mauaji kimepungua kwa asilimia 37, amesema rais huyo.

"Zaidi ya hayo, mamlaka zimekamata zaidi ya tani 300 za dawa za kulevya na kubomoa takriban maabara za siri 1,700 katika kipindi hicho," amesema.

Rais Sheinbaum amesema Mexico inaendelea kudumisha ushirikiano na Marekani katika maeneo kama vile mafunzo, kubadilishana taarifa na hatua nyingine za kudhibiti magendo ya dawa za kulevya, lakini ushirikiano huo unafanywa kwa kuzingatia kanuni za kuheshimiana na bila kutii upande mwingine.

Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum akizungumza kwenye mkutano wake na waandishi wa habari huko Mexico City, mji mkuu wa Mexico, Januari 5, 2026. (Picha na Francisco Canedo/Xinhua)

Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum akihudhuria mkutano na waandishi wa habari huko Mexico City, mji mkuu wa Mexico, Januari 5, 2026. (Picha na Francisco Canedo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha