Lugha Nyingine
Uchumi wa Kenya wakua kwa asilimia 4.9 katika robo ya tatu ya 2025
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) imesema uchumi wa Kenya umekua kwa asilimia 4.9 katika robo ya tatu ya mwaka 2025 ikilinganishwa na asilimia 4.2 ya kipindi kama hicho mwaka 2024.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na KNBS jana Jumanne, ukuaji huo unatokana na kuboreshwa kwa ufanisi katika sekta kadhaa muhimu, zikiwemo za kilimo, uzalishaji viwandani na usafirishaji, ambapo sekta za kilimo, misitu na uvuvi zimekuwa na ongezeko la asilimia 3.2 katika robo hiyo.
Taarifa hiyo imesema, sekta ya uzalishaji viwandani ilikua kwa asilimia 2.5, hata hivyo imeeleza kuwa ukuaji huo ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na mambo mchanganyiko, hasa sekta ndogo ya bidhaa zisizo za chakula.
Kwa mujibu wa KNBS, sekta ya usafirishaji na uhifadhi ilikua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 4.6 ya kipindi kama hicho mwaka 2024.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



