Lugha Nyingine
Rais wa Mali asema nchi yake inaunga mkono bila kuyumba kanuni ya kuwepo kwa China Moja
Rais Assimi Goita wa Mali amesema nchi yake itaendelea kuunga mkono bila kuyumbayumba kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani.
Rais Goita ametoa kauli hiyo jana Jumanne wakati alipopokea hati ya utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa China nchini humo Bw. Li Xiang.
Rais Goita amesema Mali na China zinashikilia maadili yanayofanana na kuwa na misimamo inayolingana kuhusu masuala makuu kama vile kuheshimu mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kupinga kuyatumia kama nyenzo na kisiasa masuala ya haki za binadamu, akisisitiza kuwa Mali itaendelea kuunga mkono bila kuyumbayumba kanuni ya kuwepo kwa China moja.
Amesema Mali ina nia ya kushirikiana na China katika kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili na matokeo yaliyopatikana katika mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kuhimiza utekelezaji wa miradi mingi zaidi ya ushirikiano wa kivitendo nchini Mali, na kuleta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



