Lugha Nyingine
Marekani kudhibiti mauzo ya mafuta ya Venezuela kwa muda usio na kikomo
Waziri wa Nishati wa Marekani Chris Wright amesema Marekani si tu itauza mafuta yaliyohifadhiwa nchini Venezuela, bali pia itadhibiti mauzo ya mafuta yanayozalishwa nchini humo kwa muda usio na kikomo.
Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa mafuta huko Miami Florida Wright jana Jumatano amesema mauzo hayo yatafanywa na serikali ya Marekani na mapato yatahifadhiwa kwenye akaunti zinazodhibitiwa na serikali ya Marekani.
Pia ameongeza kuwa mapato yanayotokana na mafuta hayo baadaye yanaweza kurudi Venezuela ili kunufaisha raia wa huko, wakati huohuo Marekani inahitaji kuwa na uwezo na udhibiti wa mauzo hayo ya mafuta ili kuendesha mabadiliko ambayo lazima yatokee nchini Venezuela.
Kwa mujibu wa maelezo ya Wright, serikali ya Trump "inafanya mazungumzo" na viongozi wa Venezuela pamoja na kampuni za mafuta za Marekani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



