China yasema udhibiti wake wa mauzo ya nje ya bidhaa zenye matumizi mawili kwa Japan ni halali,  wa haki na wa kisheria kabisa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 08, 2026

BEIJING - Hatua za China za kudhibiti mauzo ya nje ya bidhaa zenye matumizi mawili kwa Japan ni halali, za haki na za kisheria kabisa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning amesema siku ya Jumatano.

Mao amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba kauli zenye makosa za Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi kuhusu Taiwan zilikiuka mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China, kuingilia waziwazi masuala ya ndani ya China na kutishia kutumia nguvu dhidi ya China.

"Kwa lengo la kulinda usalama na maslahi ya taifa pamoja na kutekeleza wajibu wa kutoeneza silaha na mwingine wa kimataifa, China imechukua hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni," msemaji Mao amesema, akiongeza kuwa hatua hizo ni halali, za haki na za kisheria kabisa.

"Tunaitaka Japan ikabiliane na chanzo kikuu cha suala hilo, kujichunguza kwa kina, kurekebisha makosa yake na kuzirudisha nyuma kauli hizo zenye makosa za Takaichi," msemaji huyo amesema.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha