Lugha Nyingine
China yalenga usambazaji salama na wa kuaminika wa teknolojia muhimu za AI ifikapo 2027
Watu wakitembelea ukumbi wa maonyesho wakati wa Mkutano wa 5G + Intaneti ya Kiviwanda wa China 2025 mjini Wuhan, Mkoani Hubei, katikati mwa China, Novemba 21, 2025. (Xinhua/Du Zixuan)
BEIJING - China inalenga kufikia usambazaji salama na wa kuaminika wa teknolojia muhimu za Akili Bandia (AI) ifikapo mwaka 2027, huku ukubwa wa sekta hiyo na kiwango cha uwezeshaji wake vikibaki miongoni mwa mstari wa mbele duniani, kwa mujibu wa mpango kazi uliotolewa hivi karibuni wa serikali.
Mpango kazi huo, uliotolewa kwa pamoja na idara nane zikiwemo Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari, Mamlaka ya Mtandao ya China, na Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi, unaelezea msukumo mkubwa wa kufungamanisha kwa kina AI na sekta ya uzalishaji, kukuza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora na kuwezesha mchakato mpya ya viwanda kwa pande zote.
Kufikia mwaka 2027, mpango kazi huo unalenga matumizi ya kina ya mifumo mikubwa mitatu hadi mitano ya AI yenye matumizi ya jumla katika sekta ya viwanda, kuendeleza mifumo mikubwa mahsusi kwa sekta mbalimbali katika maeneo yote, kuunda seti 100 za data za viwanda zenye sifa bora, na kuhimiza hali 500 za mfano za matumizi.
Pia unalenga kukuza kampuni mbili hadi tatu zenye ushawishi mkubwa duniani zinazoongoza katika mfumo wa ikolojia, kundi la kampuni ndogo na za kati zilizo maalum na za hali ya juu, pamoja na kundi la watoa huduma wa kuwezesha wenye utaalamu wa teknolojia ya AI na ufahamu wa mambo ya sekta hiyo.
Aidha, China inapanga kujenga mfumo wa ikolojia wa chanzo huria unaoongoza duniani, kuimarisha uwezo wa usimamizi wa masuala ya usalama, na kutoa suluhisho za China katika maendeleo ya AI duniani.
Nyaraka hiyo inaelezea hatua zikiwemo za kuhimiza maendeleo yaliyoratibiwa ya vifaa na programu za chipu za AI, kuunga mkono uvumbuzi katika mbinu za kufundisha mifumo na utoaji wa matokeo, kukuza mifumo mikubwa muhimu mahsusi kwa sekta, na kuingiza kwa kina teknolojia ya mifumo mikubwa katika michakato ya msingi ya uzalishaji.
Mpango kazi huo pia unasisitiza kufikia mafanikio mapya katika teknolojia muhimu kama vile ulinzi wa usalama kwa algoriti za mifumo ya viwanda na ulinzi wa data za kufundisha mifumo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



