Lugha Nyingine
Hamas yaanza tena kutafuta mwili wa mateka wa mwisho wa Israeli huko Gaza

Wafanyakazi kutoka Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu wakitafuta mwili wa mateka wa mwisho wa Israeli mashariki mwa makazi ya Zeitoun, kusini mashariki mwa Mji wa Gaza, Januari 7, 2026. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)
GAZA - Mtu aliyetoa habari hiyo wa Hamas amesema, kundi hilo limeanza tena kutafuta mwili wa mateka wa mwisho wa Israeli aliyekuwa akishikiliwa katika Ukanda wa Gaza, ambapo mtu huyo asiyetaka kudokeza jina lake alizungumza jana Jumatano na Shirika la Habari la China, Xinhua akisema utafutaji huo unafanyika kwenye makazi ya Zeitoun, kusini mashariki mwa Mji wa Gaza, kwa ushiriki wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC).
Aliyetoa habari ameeleza kuwa, shughuli hiyo ya utafutaji inakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na uharibifu mkubwa uliosababishwa na operesheni za kijeshi za Israeli wakati wa vita, pamoja na ukosefu wa zana na vifaa muhimu.
Kituo cha Televisheni cha Kan TV News cha serikali ya Israeli pia kimeripoti juhudi hizo zilizoanza tena za Hamas na ICRC za kuupata mwili huo wa polisi wa Israeli Ran Gvili.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kunukuliwa na kituo hicho cha televisheni akisema kwamba Israeli "haitafungua tena kituo cha kuvukia mpaka cha Rafah hadi mwili wa Gvili utakaporudishwa."

Wafanyakazi kutoka Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu wakitafuta mwili wa mateka wa mwisho wa Israeli mashariki mwa makazi ya Zeitoun, kusini mashariki mwa Mji wa Gaza, Januari 7, 2026. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

Wanamgambo wa Hamas wakitafuta mwili wa mateka wa mwisho wa Israeli mashariki mwa makazi ya Zeitoun, kusini mashariki mwa Mji wa Gaza, Januari 7, 2026. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

Wanamgambo wa Hamas wakitafuta mwili wa mateka wa mwisho wa Israeli mashariki mwa makazi ya Zeitoun, kusini mashariki mwa Mji wa Gaza, Januari 7, 2026. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma