Mvua kubwa yasababisha vifo vya watu 11 nchini Madagascar

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 08, 2026

Watu wakiwa wamepanda mkokoteni ili kupita kwenye maji ya mafuriko huko Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, Januari 7, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Watu wakiwa wamepanda mkokoteni ili kupita kwenye maji ya mafuriko huko Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, Januari 7, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

ANTANANARIVO - Ripoti iliyotolewa Jumanne na Ofisi ya Kitaifa ya Usimamizi wa Hatari na Maafa ya Madagascar imeeleza kuwa mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha nchini humo tangu mwishoni mwa Novemba mwaka jana imesababisha vifo vya watu 11 na kuacha wengine sita wakiwa wamejeruhiwa.

Ofisi hiyo imesema mji mkuu, Antananarivo, ni moja kati ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi ambapo jumla ya watu 274 wameathiriwa, na nyumba 26 za makazi zimeharibiwa au kubomolewa.

Comuna ya Miji ya Antananarivo imewahimiza watu wote kuendelea kuwa na macho na kuwataka familia zote zinazoishi katika nyumba za jadi za zamani au zisizo salama kuhama kwenda maeneo salama.

Shirika la hali ya hewa la Madagascar lilisema Jumanne kwamba hali ya mvua itaendelea katika sehemu ya kaskazini magharibi na nyanda za juu za kati mwa nchi hiyo katika siku zijazo, na linatabiria kuwa mvua pia itaathiri maeneo ya kusini.

Madagascar ambayo iko magharibi mwa Bahari ya Hindi, kwa kawaida hupata msimu wake wa mvua kuanzia Novemba hadi Machi. Hali mbaya ya hewa inayoambatana nayo mara nyingi husababisha vifo vya watu, wakazi kukimbia nyumba zao, na mafuriko kwenye maeneo mengi ya ardhi ya kilimo.

Watu wakivuka barabara iliyofurika maji kwenye mtaa mmoja mjini Antananarivo, Madagascar, Januari 7, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Watu wakivuka barabara iliyofurika maji kwenye mtaa mmoja mjini Antananarivo, Madagascar, Januari 7, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Wachuuzi wakiuza matunda kando ya barabara iliyofurika maji kwenye mtaa mjini Antananarivo, Madagascar, Januari 7, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Wachuuzi wakiuza matunda kando ya barabara iliyofurika maji kwenye mtaa mjini Antananarivo, Madagascar, Januari 7, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Watu wakitembea kupitia maji ya mafuriko kwenye mtaa mjini Antananarivo, Madagascar, Januari 7, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

Watu wakitembea kupitia maji ya mafuriko kwenye mtaa mjini Antananarivo, Madagascar, Januari 7, 2026. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha