Lugha Nyingine
Kuielewa China | Ajenda na malengo ya Mpango wa 15 wa Miaka Mitano
Uundaji wa kisayansi na utekelezaji wa kuendelea bila kukoma wa mipango ya miaka mitano ni njia muhimu ambazo kwazo Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kinatawala nchi, na dirisha muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kuielewa vyema njia ya China kuelekea maendeleo ya mambo ya kisasa.
People's Daily Online imezindua "Kuielewa China," kipindi kipya ambacho kinajikita katika Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030). Sehemu mfululizo za kipindi hiki zinachambua kwa kina mipango ya maendeleo, fursa, na mbinu ya utawala ya China, ukilenga kufafanua dhana potofu na kuongeza kuelewana na kutambuana.
Katika sehemu hii ya kipindi cha "Kuielewa China," Profesa Gong Jiong kutoka Chuo Kikuu cha Biashara na Uchumi wa Kimataifa anashiriki katika mazungumzo na John Quelch, Makamu Mkuu Mtendaji wa Chuo Kikuu cha Duke Kunshan na mpokeaji wa Tuzo ya Fedha ya Shanghai Magnolia ya 2012.
Kwa pamoja, wanatoa uchambuzi wa kina wa mwelekeo wa maendeleo wa China na malengo makuu kwa miaka mitano ijayo. Wakizungumzia wasiwasi wa nje kuhusu maendeleo ya haraka ya China, wasomi hao wote wawili wanaelezea mkakati wa China wa kujikita katika kusimamia mambo yake yenyewe kwa ufanisi huku ikichangia fursa za maendeleo na nchi kote duniani. Pia wanazungumzia njia za kupita kwa China na Marekani ili kuishi pamoja na kushirikiana kwa njia ya kiujenzi.
"Mchakato wa kupanga nchini China wakati wote umekuwa muhimu sana ukiwa ni sehemu ya mafanikio ya nchi," Quelch anabainisha. Amesisitiza kwamba mipango hiyo kiudhahiri inawasilisha ajenda na malengo ya maendeleo ya China kwa dunia, ikionyesha kiwango cha juu cha uwazi na ufunguaji mlango katika njia ya maendeleo ya China.
Katika kujibu simulizi za kimataifa zinazodai kwamba "China inaelekea kufunga mlango," Gong amesema, "Sisi ni wauzaji bidha nje wakubwa zaidi duniani. Je, inawezekanaje muuzaji bidhaa nje mkubwa zaidi duniani asifungue mlango, sivyo? Hatuwezi kumudu kutokufungua mlango."
Quelch ameongeza kuwa mabadiliko ya China kuelekea muundo wa kiuchumi unaoendeshwa na mahitaji ya ndani hayawakilishi hatua kutoka utandawazi hadi kujitenga. Badala yake, ni "mkakati sambamba": wakati ikichochea matumizi na kupanua mahitaji ya ndani, China inaendelea kuhimiza uwekezaji kwenda nje ya nchi, kuunga mkono kampuni katika "kwenda kimataifa," na kuzidisha ushirikiano wa kimataifa.
Gong ameeleza zaidi kwamba kama China inakabiliwa na kile kinachoitwa "kuzalisha kupita uwezo wa mahitaji" inapaswa hatimaye kuamriwa na soko la kimataifa. Akitolea mfano wa tasnia ya magari, amejenga hoja kwamba "Ulaya haiwezi tu kuliwekea soko uzio na kuziwekea uzio bidhaa za kuagizwa ili kulinda soko."
Quelch amesema: "Ushirikiano ni muhimu kabisa kwa ajili ya mafanikio. Kinachoonekana kuwa uzalishaji uliozidi uwezo wa mahitaji halisi ya ndani katika magari ya EV ni uwezo unaofaa kwa mahitaji ya masoko ya dunia. Kwa namna hiyo, 'uzalishaji uliozidi uwezo wa mahitaji' wa China ni zawadi kwa dunia."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



