Rais wa China atuma salamu za pongezi katika hafla ya uzinduzi wa Mwaka 2026 wa China na Afrika wa Mawasiliano ya Watu na Watu

(CRI Online) Januari 09, 2026

Rais wa China Xi Jinping jana Alhamisi alituma salamu za pongezi kwenye hafla ya ufunguzi wa Mwaka 2026 wa China na Afrika wa Mawasiliano ya Watu na Watu.

Katika barua yake, Rais Xi amesema kuandaa mwaka wa mawasiliano ya watu na watu katika wakati wa kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Afrika ni maafikiano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa pande zote mbili, na inaashiria hatua muhimu katika kuimarisha zaidi uungaji mkono wa umma kwa urafiki kati ya China na Afrika katika hatua ya mwanzo ya kihistoria.

“Mawasiliano na kufunzana miongoni mwa ustaarabu mbalimbali vinabeba nguvu ya kuchochea bila kuchoka upigaji hatua wa ustaarabu wa binadamu vilevile amani na maendeleo ya dunia” Rais Xi amesema, huku akihimiza pande zote mbili kutumia mwaka huu kama fursa ya kuendeleza urafiki wa jadi, kuimarisha kufunzana miongoni mwa ustaarabu mbalimbali, kupanua mabadilishano kati ya watu na watu, hususan miongoni mwa vijana, kuzidisha kwa kina kubadilishana uzoefu katika utawala na kwa pamoja kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa.

Rais Xi amesema, kupitia juhudi hizo, pande hizo mbili zinaweza kuhimiza ukaribu kati ya watu zaidi ya bilioni 2.8 wa China na Afrika, kuunganisha pamoja mioyo, akili na nguvu zao, na kutoa michango mipya kwenye mshikamano wa Dunia ya Kusini katika kukabiliana na changamoto za dunia, kuhimiza maadili ya pamoja ya binadamu, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha