China, Ethiopia zaahidi kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing

(CRI Online) Januari 09, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi jana Alhamisi alikutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Gedion Timothewos mjini Addis Ababa, huku pande hizo mbili zikiahidi kusukuma mbele kwa pamoja utekelezaji wa matokeo yaliyopatikana kwenye Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa kwa wanahabari, pande hizo mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja zote na kujitahidi kujenga uhusiano wa kimkakati wa hali zote kati ya China na Ethiopia kuwa mfano wa kuigiwa kwa ajili ya kujenga Jumuiya ya hali zote ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mapya.

Pande hizo mbili zimeahidi kuimarisha ushirikiano katika nyanja za jadi, zikiwemo uchumi, biashara, miundombinu, nishati, uchukuzi na sheria, kufungua fursa za ushirikiano katika nyanja mpya kama vile biashara ya mtandaoni, uchumi wa kidijitali, Akili Mnemba na nishati ya kijani, na kupanua wigo wa ushirikiano katika utamaduni, utalii, vyombo vya habari, elimu na taasisi za washauri bingwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha