Tanzania yatarajia ukuaji imara wa uchumi mwaka 2026

(CRI Online) Januari 09, 2026

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emmanuel Tutuba amesema, uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa nguvu katika robo ya kwanza ya 2026, ukiungwa mkono na mfumuko mdogo wa bei.

Akizungumza baada ya mkutano wa Kamati ya Sera za Fedha uliofanyika Jumatano mjini Dar es Salaam, Bw. Tutuba amesema ukuaji wa uchumi katika Tanzania Bara unakadiriwa kuja kufikia asilimia 6 katika robo ya kwanza ya 2026, wakati huohuo uchumi wa Zanzibar unakadiriwa kuja kukua kwa asilimia 7.2.

Bw. Tutuba amesema ukuaji huo unaendelea kuchochewa kwa kiasi kikubwa na kilimo, madini na ujenzi, huku mfumuko wa bei ukiendelea kuwa mdogo na tulivu.

Amesema, mfumuko wa bei ulikuwa wa wastani ya asilimia 3.5 katika Tanzania Bara na asilimia 3.4 katika visiwa vya Zanzibar katika robo ya nne ya 2025, na unatarajiwa kubaki ndani ya kiwango lengwa katika mwaka mzima wa 2026.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha