China na Umoja wa Afrika zafanya mazungumzo ya kimkakati katika makao makuu ya AU

(CRI Online) Januari 09, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mahmoud Ali Youssouf wakifanya kwa pamoja Mazungumzo ya tisa ya Kimkakati kati ya China na AU kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Januari 8, 2026. (Xinhua/Han Xu)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Mahmoud Ali Youssouf kwa pamoja wamefanya Mazungumzo ya 9 ya Kimkakati kati ya China na AU kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Kwenye mazungumzo hayo yaliyofanyika jana Alhamisi, viongozi hao wamebadilishana maoni kuhusu juhudi za pamoja za China na Afrika katika kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa, usimamizi wa dunia, sera ya ushuru sifuri, Shirikisho la Kimataifa la Upatanishi, na Mtazamo wa Amani na Maendeleo katika Pembe ya Afrika.

Pande zote mbili zimesema China na Umoja wa Afrika, zikiwa sehemu ya Dunia ya Kusini, zina mtazamo sawa katika masuala makubwa ya kimataifa na ya kikanda. Zimeeleza umuhimu wa kulinda kwa pamoja haki na maslahi halali ya Dunia ya Kusini.

Pia pande zote mbili zimesisitiza haja ya kudumisha utaratibu wa kimataifa kwa msingi wa sheria ya kimataifa, hususan katika kuheshimu mamlaka huru na ukamilifu wa ardhi, vilevile utatuzi wa amani wa migogoro.

Viongozi hao pia wamebadilishana maoni kuhusu ushirikiano katika nyanja mbalimbali, ikiwemo juhudi za pamoja za China na Afrika katika kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha