Lugha Nyingine
Russia yasema Marekani haipaswi kuzuia kurudishwa kwa haraka raia wake walio kwenye meli ya mafuta iliyokamatwa
(CRI Online) Januari 09, 2026
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema Marekani haipaswi kuzuia kurejeshwa kwa haraka raia wake walio kwenye meli ya mafuta iliyokamatwa na Marekani ikiwa inapeperusha bendera ya Russia.
Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo leo Ijumaa inasema kuwa kwa kuzingatia taarifa kuhusu uwepo wa raia wa Russia miongoni mwa wafanyakazi wa meli hiyo, Russia inaisihi Marekani kuhakikisha raia wake wanatendewa kibinadamu na kwa heshima, kuheshimu kikamilifu haki na maslahi yao, na kutozuia kurejea kwao nyumbani kwa haraka.
Mapema jana Alhamisi Wizara ya Uchukuzi ya Russia ilisema meli hiyo ilipewa idhini ya muda tarehe 24 Desemba 2025 ya kufanya safari huku ikipeperusha bendera ya taifa la Russia kwa mujibu wa sheria za Russia na za kimataifa.
(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



