Mashindano ya Kombe la Dunia Mwaka 2026 kutumia teknolojia kadhaa za kivumbuzi za AI za China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 09, 2026

Washington – Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na mshirika wake rasmi wa teknolojia, Kundi la Lenovo, wametangaza pamoja Jumatano wiki hii kwamba Mashindano ya Kombe la Dunia Mwaka 2026 ya Marekani, Canada na Mexico yatatumia teknolojia kadhaa za AI zilizobuniwa na kampuni ya China ya Lenovo, ili kuboresha teknolojia za uamuzi wa mechi na uwezo wa kuchambua mashindano na kuongeza uzoefu wa ushiriki wa mashabiki.

Habari zimesema kuwa, teknolojia za Lenovo za mfumo wa hali ya juu wa AI wenye ujuzi wa Soka, mfumo wa mwamuzi msaidizi wa video (VAR) wenye kuonesha wachezaji kidijitali kwa 3D, na mfumo wa AI wa kuongeza ubora wa picha ya video kwa mtazamo wa mwamuzi zitatumika kwenye Mashindano ya Kombe la Dunia ya Marekani, Canada na Mexico.

Aidha, Lenovo pia itategemea miundombinu ya AI ya mseto kwa kutoa teknolojia zinazohusisha kazi za kuhakikisha uwasilishaji wa zana na vifaa, huduma za uwanjani na huduma za uhifadhi kwa mashindano ya mwaka huu. Pia, itafanya usimamizi wa pamoja na usimamizi wa hali ya mambo yanayokadiriwa juu ya usafirishaji wa bidhaa zinazohusiana na mashindano, mawasiliano ya habari na hali ya uendeshaji wa mashindano haya, ili kuhakikisha uendeshaji wa mashindano unaendelea kwa ufanisi wa juu, salama na kwa kufuata utaratibu katika kila eneo la mashindano.

Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema kwamba, “Mashindano ya Kombe la Dunia Mwaka 2026 yatakuwa mashindano makubwa zaidi katika historia, FIFA na Lenovo zinakumbatia teknolojia za dijitali na AI katika sehemu zote, hii si kutoa tu uungaji mkono kwa timu na waamuzi, pia kuleta uzoefu mpya wa kushangaza kwa mashabiki wote.”

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha