China na Lesotho zaapa kusukuma mbele ushirikiano wa kimkakati hadi ngazi ya juu zaidi

(CRI Online) Januari 12, 2026

(Picha inatoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.)

(Picha inatoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.)

Lesotho na China zimethibitisha tena dhamira yao ya kusukuma mbele ushirikiano wa kimkakati wa pande mbili hadi ngazi ya juu na kuufanya kuwa mfano wa mawasiliano ya kirafiki na maendeleo ya pamoja kati ya nchi zenye hali na mifumo tofauti ya kitaifa.

Hayo yamo kwenye taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Jumapili, kufuatia mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi aliyefanya ziara nchini humo Jumamosi na Jumapili, na mwenzake Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Lesotho Lejone Mpotjoana huko Maseru, nchini Lesotho.

Taarifa imesema mawaziri hao wamesifu mafanikio ya maendeleo ya uhusiano wa pande mbili, na kuongeza kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kuungana mkono kwa dhati kwenye masuala yanayohusu maslahi yao ya msingi na yanayofuatilia zaidi na kila mmoja.

Mawaziri hao wamezungumzia matokeo muhimu yaliyopatikana katika hatua 10 za ushirikiano ambazo China na Afrika zimechukua kwa pamoja ili kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa.

Mawaziri wote wawili wana imani kwamba mabadiliko ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita yanashika kasi, na nchi za Kusini mwa Dunia zina jukumu muhimu zaidi katika masuala ya kimataifa.

(Picha inatoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.)

(Picha inatoka tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China.)

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha