Lugha Nyingine
China na Afrika Kusini zatoa wito wa ushirikiano wa karibu kati ya Kusini na Kusini
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye kwa sasa yupo ziarani katika nchi za Afrika, alifanya mazungumzo kwa njia ya simu Jumamosi na mwenzake wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, akitoa wito kwa nchi zote mbili kuunga mkono mifumo ya pande nyingi na kuimarisha ushirikiano kati ya Kusini na Kusini.
Wang, amekipongeza chama tawala cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC) kwa maadhimisho ya miaka 114 tangu kuanzishwa kwake, akielezea imani kwamba kupitia juhudi za pamoja za ANC, Afrika Kusini itaungana kukabiliana usumbufu kutoka nje na kufikia maendeleo na ustawi wa kitaifa.
“China iko tayari kudumisha mabadilishano ya ngazi ya juu na Afrika Kusini, kupanua mawasiliano baina ya vyama, kuimarisha kuaminiana kimkakati na kuzidisha ushirikiano wa kivitendo,” Wang amesema, akibainisha kuwa China itawezesha utekelezaji nchini Afrika Kusini wa hatua zake za kutoza ushuru-sifuri kwa Afrika na kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi ya Afrika Kusini, ili kuleta manufaa kwa watu wa Afrika Kusini.
Kwa upande wake Lamola amekaribisha ziara hiyo ya Wang barani Afrika katika Mwaka Mpya na kuishukuru China kwa kuiunga mkono Afrika Kusini kuandaa Mkutano wa Viongozi wa G20 na kwa uungaji mkono wake katika kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi za Afrika, ikiwemo Afrika Kusini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



