Wizara ya Biashara ya China kuhimiza zaidi matumizi na ufunguaji mlango katika Mwaka 2026

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 12, 2026

Mmiliki wa duka akipanga Qipao, gauni la kijadi la wanawake wa China, kwenye duka katika Eneo la Qilihe la Lanzhou, Mkoa wa Gansu, kaskazini magharibi mwa China, Januari 6, 2026. (Xinhua/Chen Bin)

Mmiliki wa duka akipanga Qipao, gauni la kijadi la wanawake wa China, kwenye duka katika Eneo la Qilihe la Lanzhou, Mkoa wa Gansu, kaskazini magharibi mwa China, Januari 6, 2026. (Xinhua/Chen Bin)

BEIJING - Mkutano wa siku mbili wa kitaifa wa China wa kazi ya biashara uliomalizika jana Jumapili umesema kwamba Wizara ya Biashara ya China itaifanya kazi yake ya kuhimiza zaidi matumizi na kupanua ufunguaji mlango kuwa moja ya kazi zake muhimu za mwaka 2026.

Mkutano huo umeeleza kuwa, mfumo wa biashara wa kitaifa wa China utafanya shughuli za kuchochea matumizi, kujenga chapa ya "Fanya Manunuzi China" kwa kupitia kuhimiza ongezeko jipya la matumizi ya huduma, na kuboresha sera za kutoa ruzuku kwa wanunuzi kununua bidhaa mpya kwa kubadilishana na za zamani kwa bidhaa za matumizi.

Kwa lengo hili, mkutano huo pia umesisitiza matumizi ya kidijitali, kijani, na matumizi ya bidhaa husika za afya, na kusisitiza pia nguvu ambayo bado haijatumika katika masoko yanayoibuka kote nchini.

Kuhusu biashara, mkutano umeeleza kuwa juhudi zitafanywa kwa kuboresha biashara ya bidhaa, kupanua biashara ya huduma na mauzo ya nje, na kuhimiza biashara ya kidijitali na ya kijani ili kujenga chapa ya "Kuagiza Bidhaa za Nje kwenda China".

Ili kuvutia uwekezaji kutoka nje na kung'arisha chapa ya "Wekeza China", China itaimarisha ufunguaji mlango katika shughuli za huduma, kuboresha uhamasishaji wa uwekezaji, na kukamilisha utaratibu wa huduma kwa kampuni za biashara za kigeni.

Ili kupanua ufunguaji mlango, mkutano huo umesema China itaendana na sheria za biashara za kimataifa za vigezo vya juu, kuboresha maeneo ya majaribio ya biashara huria na Bandari ya Biashara Huria ya Hainan, na kuandaa maonyesho muhimu kwa matokeo halisi.

Ili kufanya vizuri zaidi usimamizi wa uwekezaji wa nje, zitachukuliwa hatua nyingi zaidi za kuongoza mpangilio wa kuvuka mpaka wa minyororo ya utoaji bidhaa wa viwanda, kuimarisha mitandao ya huduma za ng'ambo, kuzidisha ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na kuimarisha usimamizi wa hatari.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha