Lugha Nyingine
Maandamano kadhaa dhidi ya ICE yafanyika kote Jimbo la California, Marekani

Watu wakishiriki kwenye maandamano dhidi ya Idara ya Uhamiaji na Usimamizi wa Forodha (ICE) mjini Pasadena, Kaunti ya Los Angeles, California, Marekani, Januari 10, 2026. (Xinhua)
LOS ANGELES - Kutoka mji mkuu wa California, Sacramento hadi mji wa Sonora, na kutoka San Francisco hadi Los Angeles, maandamano kadhaa dhidi ya Idara ya Uhamiaji na Usimamizi wa Forodha (ICE) yamefanyika kote jimbo la California siku ya Jumamosi.
Maandamano hayo, yaliyopewa jina la "ICE OUT For Good," yaliandaliwa na mtandao wa makundi mbalimbali, yakiwemo Muungano wa Haki za Kiraia za Marekani na Vuguvugu la 50501, ambalo liliandaa maandamano makubwa katika majimbo yote 50 ya Marekani karibu kila mwezi mwaka jana.
Huko Pasadena, mji jirani na Los Angeles, waandamanaji zaidi ya 500 walikusanyika katika kona iliyo karibu na ukumbi wa mji, wakitoa kaulimbiu za "Hapana ICE, Hapana KKK, Hapana Marekani ya Kifashisti," huku honi za magari na vifijo vikisikika.
Kwa mujibu wa taarifa ya Vuguvugu la 50501 iliyotolewa Ijumaa, angalau watu 32 walifariki wakiwa chini ya ulinzi wa ICE mwaka 2025.
Hatua hizo za Jumamosi zilifuatia matukio mawili ya hivi karibuni -- ofisa wa serikali kuu kumpiga risasi na kumuua Renee Good, mama wa watoto watatu mwenye umri wa miaka 37 huko Minneapolis, pamoja na tukio lingine ambalo askari mwingine kuwapiga risasi na kuwajeruhi watu wawili huko Portland, Oregon mapema wiki iliyopita.
"Tuko hapa kutambua kwamba nchi hii inahitaji kubadili mwelekeo wake, na tunawahamasisha raia wa jamii za milima ya San Gabriel kujiunge nasi katika maandamano. Sababu maalum ni kuomboleza kifo cha mwanamke asiye na hatia aliyepoteza maisha yake kwa ajili ya harakati," mwanaharakati Dias Alan ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua Jumamosi.
Mwandamanaji wa kike, mhamiaji kutoka Australia ambaye alijitambulisha kwa jina lake la kwanza pekee kama Jenny, ameliambia Xinhua kwamba alitazama video nyingi kuhusu tukio la Minneapolis.
"ICE ni tishio kwa usalama wa umma. Hili ni tishio kwa sisi sote wahamiaji." Amesema.

Watu wakishiriki katika mkesha wa kumuomboleza Renee Good, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na askari wa Idara ya Uhamiaji na Usimamizi wa Forodha (ICE), mjini Carson, Kaunti ya Los Angeles, California, Marekani, Januari 10, 2026. (Xinhua)

Mwandamanaji aliyeshikilia bango akishiriki katika maandamano dhidi ya Idara ya Uhamiaji na Usimamizi wa Forodha (ICE) mjini Pasadena, Kaunti ya Los Angeles, California, Marekani, Januari 10, 2026. (Xinhua)

Mwandamanaji aliyeshikilia bango akishiriki katika maandamano dhidi ya Idara ya Uhamiaji na Usimamizi wa Forodha (ICE) mjini Pasadena, Kaunti ya Los Angeles, California, Marekani, Januari 10, 2026. (Xinhua)

Mwandamanaji aliyeshikilia bango akishiriki katika maandamano dhidi ya Idara ya Uhamiaji na Usimamizi wa Forodha (ICE) mjini Pasadena, Kaunti ya Los Angeles, California, Marekani, Januari 10, 2026. (Xinhua)

Watu wakishiriki katika maandamano dhidi ya Idara ya Uhamiaji na Usimamizi wa Forodha (ICE) mjini Pasadena, Kaunti ya Los Angeles, California, Marekani, Januari 10, 2026. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



