Lugha Nyingine
Trump aitishia Cuba akiitaka “ifikie makubaliano na Marekani kabla ya haijachelewa”
(CRI Online) Januari 12, 2026
Rais Donald Trump wa Marekani ameongeza shinikizo dhidi ya Cuba, akiitishia nchi hiyo kuwa hakutakuwa na mafuta au fedha itakayoingia nchini humo huku akipendekeza "ifikie makubaliano na Marekani, mapema kabla haijachelewa.”
“Cuba imekuwa, kwa miaka mingi, ikitegemea kiasi kikubwa cha mafuta na fedha kutoka Venezuela" Rais Trump ameandika jana Jumapili kwenye jukwaa lake la mtandao wa kijamii la Truth Social.
Katika ujumbe wake huo Trump hata hivyo hakueleza ni makubaliano gani hasa ambayo anaitaka Cuba kuyafikia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



