Ethiopia yaweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja wa ndege mkubwa zaidi barani Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 12, 2026

Mesfin Tasew, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Kampuni za Ndege la Ethiopia, akizungumza kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi  la ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika Jimbo la Oromia nchini Ethiopia, Januari 10, 2026. (Kundi la Kampuni za Shirika la Ndege la Ethiopia/kupitia Xinhua)

Mesfin Tasew, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Kampuni za Ndege la Ethiopia, akizungumza kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika Jimbo la Oromia nchini Ethiopia, Januari 10, 2026. (Kundi la Kampuni za Shirika la Ndege la Ethiopia/kupitia Xinhua)

ADDIS ABABA - Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed juzi Jumamosi alizindua rasmi ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, ambao baada ya kukamilika kwake, unatarajiwa kuwa kituo kikubwa zaidi cha usafiri wa anga barani Afrika.

Waziri mkuu huyo, akiambatana na maofisa waandamizi wa serikali, aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa uwanja huo karibu na mji wa Bishoftu katika Jimbo la Oromia, umbali wa kilomita takriban 40 kusini-mashariki mwa mji mkuu, Addis Ababa.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Abiy alisema mradi huo wa uwanja mkubwa wa ndege ni sehemu ya mkakati mpana wa Ethiopia wa kudumisha ukuaji wa haraka wa usafiri wa anga na kuimarisha nafasi ya nchi hiyo ya kuwa lango kuu la usafiri wa anga barani Afrika.

"Ninapenda kuwapongeza wote kwa kuwepo katika siku hii kubwa na kushiriki kwenye hafla ya furaha kama hii inayoonesha mwanzo wa hatua ya Ethiopia kuelekea mambo ya kisasa, ustawi na uchangamfu kwa mabadiliko," Abiy alisema.

Ameeleza kuwa baada ya miaka minne ujenzi wa kipindi cha kwanza utakamilika, ambapo uwanja huo mpya wa ndege utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 60 kwa mwaka. Na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi mzima, uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 110 kwa mwaka.

Waziri Mkuu huyo amesema kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Addis Ababa Bole (uliopo sasa), ambao una uwezo wa kuhudumia abiria wapatao milioni 25 kwa mwaka, hivi karibuni utafikia kikomo chake cha juu cha uwezo kwa kasi ya ukuaji wa sasa.

"Katika kipindi cha kwanza cha ujenzi wa mradi wa uwanja mpya wa ndege, vitajengwa vituo viwili vikubwa vya abiria, njia mbili za kurukia na kutua ndege, maeneo yenye uwezo wa kuegesha ndege 180, hoteli moja, kituo cha uchukuzi wa mizigo ambacho kinaweza kushughulikia tani milioni 1.5 za bidhaa kwa mwaka, na pia karakana ya utengenezaji wa ndege," amesema Mesfin Tasew, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Kampuni za Ndege la Ethiopia.

Tasew amesema mradi huo wa kipindi cha kwanza pia unahusisha ujenzi wa barabara kuu ya kisasa yenye njia mbalimbali za magari inayounganisha uwanja huo mpya wa ndege na Addis Ababa, na pia itajenga njia ya reli ya mwendo kasi yenye urefu wa kilomita 38 ya kupitisha treni kwa kasi ya kilomita 120 hadi 200 kwa saa. 

Picha hii iliyopigwa Januari 10, 2026 ikionyesha eneo la ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika Jimbo la kikanda la Oromia la Ethiopia, Januari 10, 2026. (Kundi la Kampuni za Shirika la Ndege la Ethiopia/kupitia Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Januari 10, 2026 ikionyesha eneo la ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bishoftu, karibu na mji wa Bishoftu katika Jimbo la Oromia la Ethiopia, Januari 10, 2026. (Kundi la Kampuni za Shirika la Ndege la Ethiopia/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha